5/05/2022

TARURA yaondolewa kukusanya ushuru wa maegesho

 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Innocent Bashungwa ameagiza kazi ya kukusanya ushuru wa maegesho ya magari, iliyokua chini ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (Tarura) irudishwe kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.


Waziri Bashungwa ametoa maagizo hayo leo, wakati wa Kikao chake na Uongozi wa Tarura na mawakala wa ukusanyaji ushuru wa maegesho kwenye halmashauri mbalimbali nchini.


Pia amemuelekeza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Prof. Riziki Shemdoe kusimamia makabidhiano ya chanzo hicho haraka baina ya Tarura na Mamlaka za Serikali za Mitaa.


“Naona malalamiko kutoka kwa wananchi hayaishi kuhusiana na chanzo hiki na Rais wetu Samia Suluhu Hassan hafurahishwi na malalamiko haya ya wananchi kila mara”.


“Pia hili la ukusanyaji wa parking sio jukumu la msingi la Tarura, hivyo nalirudisha halmashauri, ili ninyi Tarura mkasimamie kutengeneza barabara na miundombinu kama hiyo,”amesema Waziri Bashungwa


Ameongeza kuwa: “Nitapenda kuona sasa Tarura mkielekeza nguvu kwenye kuimairisha miundombinu ya barabara za mijini na vijijini na mkafungue barabara na kufika kusikofikika, madaraja yakajengwe, makalavati ili kurahisisha usafiri kwa wanannchi wetu,” amesema.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger