5/03/2022

TCRA Yachunguza Malalamiko Kuhusu Vifurushi vya Simu

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Baada ya malalamiko mitandaoni kuwa Kampuni za Mawasiliano ya Simu Nchini Tanzania zimefanya mabadiliko na kupandisha gharama za vifurushi vya intaneti bila kutoa taarifa kwa Wateja wao, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema inafuatilia

TCRA imesema "Tumeona malalamiko kutoka kwa Wadau mtandaoni kuwa watoa huduma wa Mitandao ya Simu wamebadilisha vifurushi kimya kimya, endapo kuna mtumiaji amenunua kifurushi, halafu akapata tofauti na kile alicholipia, awasiliane nasi. Mamlaka inafuatilia suala hili kwa watoa huduma ili kuweza kubaini ukweli"


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

1 comment:

  1. Kwani nyie hamnunui mkaona hadi wadau wathibitishe??

    ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger