Tems Ashika Namba Moja Kwenye Billboard hot 100

 NAFASI ZA AJIRA BONYEZA HAPATemilade Openiyi, anayejulikana zaidi kwa jina la Kisanii Tems, nyota wa Nigeria, ambaye ameingia kwenye rekodi ya kuwa msanii wa kwanza wa Nigeria katika historia, kwa mara ya kwanza kuishika namba moja kwenye chati za Billboard Hot 100.

Safari ya mwanamuziki huyo nje ya mipaka ya Afrika ilianza kushamiri zaidi mwaka jana 2021, ambapo ushirikiano wake na mwimbaji Wizkid ulimpenyeza mpaka kwenye hit 10 bora zaa Billboard kupiti wimbo maarufu ‘Essence’.

Wakati huo Wizkid aliishikilia rekodi ya kuwa mwanamuziki wa kwanza wa Kiafrika kuwa na wimbo ndani ya chati ya 10 bora za Billboard..

Miezi kadhaa baadaye, Tems anapata nafasi ya kushirikishwa katika wimbo ‘Wait For U’ unaopatikana kwenye album mpya ya msanii nyota kutoka nchini Marekani Future iitwayo ‘I Never Liked You’ ambayo ndani yake ameshirikishwa rapa Drake pia.

Rekodi hii inakuwa sehemu ya safari nyingine njema kwa Tems baada ya kushika nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard Hot 100 na kumfanya kuandika historia ya kuwa mwanamuziki wa kwanza wa Nigeria kuandika historia hiyo.


Unapenda Simulizi za Kusisimua?

Kuna Simulizi ya NDOA YANGU na kuna INATOSHA, Zitakukosha sanaa.
Bofya HAPA kufurahia sehemu ya 1 bure ndani ya group la telegram.


 

 JINSI YA KUANDIKA CV BORA BONYEZA HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad