5/14/2022

Ukweli Mchungu...Asilimia Kubwa Ndugu Huvunja Ndoa za Ndugu zao

 


Tubadilike mtu akishaoa au akiolewa waacheni waishi maisha yao,watu wameoana tayari mshaenda kujazana kuishi hapo mara bibi,sijui shangazi,sijui shemeji,acheni wanandoa waishi kwa uhuru mnawabana, mara waletewe mtoto sijui wa nani walee ,acheni wanandoa waishi wenyewe kusalimiana iwe mara moja moja na mtoe taarifa sio kwenda tu kama kwenu.


Ndugu mnachangia sana wanandoa kuachana kwa sababu mkishaenda kukaa mnaanza maneno na chokochoko. Watu wakioana waacheni waishi maisha Yao wapeni uhuru,wapeni nafasi.


Kina mama wengi wanavunja ndoa za watoto wao kwa kuingilia na kuanza kuwapangia wanandoa waishi namna gani ,wazae watoto wangapi? Kina mama kuweni busy na maisha yenu maisha ya wanandoa hayawahusu nyie wabarikini inatosha sio kuanza kuchongoa midomo na wivu wivu usio na maana,eti kisa umemzaa kwa uchungu ndio umpangie maisha haitakiwi


Nimegundua ndoa nyingi huvunjika kisa ndugu,kwenda kujirundika kukaa kaa tu kwa watu wameoana

Tubadilike

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger