Urusi Kukalia Majimbo Kadhaa ya Ukraine
Urusi inapanga kuchukua majimbo mawili ya Ukraine eneo la Mashariki, mwa mujibu wa afisa wa juu wa Marekani, wakati huu mapamabano yakiendelea kushuhudiwa.

Kwa mujibu wa Michael Carpenter, Balozi wa Marekani katika Shirika la ushirikiano wa usalama barani Ulaya, Urusi inampango wa kuyachukua majimbo ya Luhansk na Donetsk, ili kuwa sehemu yake mwezi huu wa Mei, kama ilivyofanya kwa Crimea mwaka 2014.

Aidha, amesema Urusi inafikiria kuchukua jimbo lingine la Kherson, ambalo wanajeshi wake wanadhibiti n ahata sarafu yake ya Ruble kuanza kutumiwa.

Wakati hayo yakijiri, Wizara ya Ulinzi ya Urusi, inasema watu zaidi ya Elfu 11 wakiwemo watoto Elfu Moja na mia nane, wameondolewa kutoka nchin Ukraine bila kuushirikisha uongozi wa Kiev.


Naye Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson anatarajiwa kutangaza msaada wa Dola Milioni 400 kuisaidia Ukraine, kuendelea kupambana na Urusi. 
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad