5/07/2022

Wakazi Achafukwa na TCRA Kuufungia Wimbo wa Mtasubiri "Uko Wapi Uhuru wa Kufanya Sanaa Kiubunifu"

 


Ameandika Msanii Wakazi Kupitia Instagram:

Video ya “Mtasubiri” ya Diamond & Zuchu, inafungiwa na BASATA na TCRA, ila sioni viongozi wa Shirikisho wala wa TUMA wakitoa kauli. 🤔

Ila zaidi, sijaona Msanii yeyote akipaza sauti kupinga swala hilo… ni kama tunakubaliana nalo, au tunafurahia akifungiwa?! 🤷🏾‍♂️


Uko wapi uhuru wetu wa kuwa wabunifu, na kufanya sanaa kiuhalisia?! Sisi ni “Kioo cha Jamii” sababu tunaakisi (reflect) yanayoendelea kwenye jamii yetu. Siku hizi tunaona watu wanaji-snap wakiwa Kanisani, na wengine hadi wana “Twerk” kabisa tena wakiwa wamevaa mavazi ambayo ni inappropriate. Leo unafungia wimbo kisa kuna dhehebu fulani limesema limekwazwa? Kwanza hao wapendwa walikuwa wanatafuta nini kwenye video ya secular music?! This is ridiculous…!! Biblia inasema “ya Kaisari mpe Kaisari, ya Mungu mpe Mungu”. Hao waliokwazwa na Diamond walikuwa wanatafuta nini kwenye video yake?


Harusi zinafungiwa makanisani na ma Camera kama yote. Kuna makanisa hadi yaliruhusu Wanasiasa kufanya siasa zao madhabahuni (Hatujasahau). Leo kijana mtafutaji anabuni Sanaa yake, mtake kumzibia rizki? SIO SAWA. Wakristo tupunguze Unafiki…!


Kwanza ningekuwa mimi ningefurahia watoto wa Kiislamu kufanya Sanaa inayowa-depict kama Wakristo, it is acknowledgement, complimentary and sign of respect. Au ndio baada ya kumuona Mufti ame kiki na “Mwezi kuandama” mmetaka kujitutumua na nyie sio.


Hayo madhehebu yaliyolalamika ni WANAFIKI ila BASATA na TCRA pia ndio bure kabisa, kwamba mnapelekeshwa na hisia za wachache badala ya kusimamia Sanaa, Ubunifu na Misingi yake. Mnaiangusha Sanaa, na mnatuangusha Wasanii.


Ila nimesikitishwa pia na ukimya wa Wasanii kwenye hili. Mwenzetu ameonewa Live, alafu sisi tunapiga kimya… ni WIVU, UOGA au USHAMBA?! Hii ni kuanzia Viongozi hadi Wasanii binafsi… Hebu tupaze sauti pamoja ili tuweze kupata Uhuru wa Sanaa na Ubunifu, ili itupatie Ujira na pia nafasi ya kushindana Kimataifa. Tunachekwa na Kutia Aibu huko duniani, na wanatushangaa jinsi ambavyo tunajiwekea vikwazo wenyewe na tunaishia kudumaa.


Yeah, run and tell them I said it!!


The Leader

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger