Wakurugenzi Watano MSD Waondolewa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametangaza kuondolewa kazini Wakurugenzi watano wa Bohari ya Dawa (MSD), kufuatilia malalamiko mengi ambayo yamekuwa yakitolewa na wabunge na wadau wengine kuhusu utendaji usioridhisha wa bohari hiyo.

Waziri Ummy Mwalimu ameliambia bunge jijini Dodoma kuwa pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kubadilisha uongozi wa juu wa MSD na kumteua mwenyekiti mpya wa bodi, hatua hiyo ilikuwa haitoshi kutokana na malalamiko mengi yaliyokuwa yakitolewa.

“Mkurugenzi wa Fedha anaondoka MSD, Mkurugenzi wa manunuzi MSD, Mkurugenzi wa Logistics MSD, Mkurugenzi wa Sheria MSD na Mkurugenzi wa Utawala wa MSD anaondoka.” amesema Waziri Ummy Mwalimu

Waziri huyo wa Afya ametangaza uamuzi huo wakati akihitimisha mjadala wa bajeti kwa wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023, baada ya kuchangiwa na wabunge mbalimbali.


Pia amesema wizara ya afya itasimamia ubora na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na kuipima MSD kwa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa miezi mitatu mitatu badala ya mwezi mmoja mmoja.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad