5/31/2022

Watatu Wauawa na Tembo Wakielekea Shambani

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Watu watatu wameua na Tembo katika kijiji cha Kilosa kwa Mpepo wilayani Malinyi mkoani Morogoro

Watu hao walikuwa wakielekea shambani ambapo kundi la wanyama hao lilivamia kijijini hapo na kusababisha mauti ya watu hao

Wakizungumza na EATV  ndugu wa marehemu wanasema kuwa nduzu zao wamekutwa na mauti wakiwa wanaelekea shambani

Waliopoteza maisha ni Colletha Gimwalasa, Geoffrey Sawasawa na mwingine ambaye hakufahamika mara moja jina lake mara moja

Wanasema changaamoto ya uvamizi wa wanyama hao imekuwa ni ya muda mrefu huku jitihada za kukabiliana nao zikikwama mara kwa mara kutokana na ukosefu wa mawasilinao baina yao na mamlaka ya usimamaizi wa wanyama pori

Wakizungumza katika mazishi ya watu hao wahifadhi kutoka TAWA wanewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na kuiomba serikali kuharakisha upatikanaji wa mtandao wa simu wa uhakika, kujengwa vituo vya ulinzi, pamoja na kurekebishwa baadhi ya barabara za kufika eneo hilo ili kuweka uharaka wa upatikanaji huduma sambamba na uokoaji pindi yanapotokea majanga ya namna hiyo

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger