5/04/2022

Waziri Aongeza Siku 4 kwa Waombaji wa Ajira Kada za Elimu na Afya


Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa @innocentbash ameongeza siku 4 kwa Waombaji wa ajira Kada za Elimu na Afya hivyo kwa sasa mwisho wa kuomba ajira hizo ni tarehe 08 Mei,2022 saa 5:59 usiku na sio tarehe 04 Mei,2022 kama ilivyotangazwa hapo awali.

Bashungwa amesema ameongeza siku hizo ili wale wote walioshindwa kukamilisha maombi yao tangu ajira hizo zilipotangazwa tarehe 20 Mei,2022 kwa sababu zozote zile kutumia muda huu wa nyongeza kukamilisha maombi yao kupitia kiunganishi cha ajira.tamisemi.go.tz

Akizungumzia idadi ya Waombaji wa ajira hizo amesema mpaka kufikia tarehe 03.05.2022 saa 5:59 usiku waombaji waliokamilisha maombi yao kupitia mfumo kwa Kada ya Afya ni 39,053 na Kada ya Elimu ni 119,133 hivyo jumla ya Waombaji wote ni 158,186.

Ofisi ya Rais - TAMISEMI ilipata Kibali cha Ajira cha Watumishi 9,800 kwa Kada ya Ualimu na 7,612 kwa Kada ya Afya na tangazo la Ajira hizo lilitolewa tarehe 20.04.2022, Waombaji walitakiwa kutuma maombi kuanzia tarehe 20 Aprili – 04 Mei,2022 hivyo kwa sasa mwisho wa kutuma maombi hayo ni tarehe 08 Mei,2022 saa 5:59 usiku.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger