5/03/2022

Waziri Nape Atoa Tahadhari Mjadala Bei za vifurushiWaziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye ametoa tahadhari kwa wanahabari kote nchini kuzingatia weledi katika kutimiza majukumu yao baada ya mtandao mmoja kuripoti kuhusu maamuzi ya watoa huduma za intaneti kushusha vifurushi kwa malipo ya gharama zilezile.

Katika akaunti yake ya Twitter nape ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kupata ushahidi kutoka Dar Mpya Blog ambayo ilichapisha taarifa hizo.

“Nadhani tuende zaidi ya hapa. Kwa kuwa Dar Mpya Blog wameeleza kuwa kuna wanaolalamika juu ya jambo hili, nawataka Dar Mpya Blog watusaidie kupata wanaoona wamedhulumiwa kwenye hili tutumie ushahidi wao kuchukua hatua dhidi ya wote kama wapo waliopandisha kinyemela,” ameandika katika ukurasa wake wa twitter.

Waziri Nape ameongeza kuwa “Kwa jinsi ilivyoandikwa inaonyesha Dar Mpya Blog wana ushahidi kuwa kuna uamuzi wa kubadili vifurushi ambao umefanywa kimyakimya , Nawataka TCRA kuwasiliana nao ili kupata ushahidi wa UAMUZI HUO.


Hata hivyo mtandao wa Darmpya blog umeweka MASAHIHISHO
“Kufuatia habari tuliyoichapisha leo, kuhusu gharama za vifurushi na kuleta taharuki, tunaomba radhi kwa kutopata maoni ya upande wa pili ambayo ni mamlaka husika (@TCRA_Tz).
Tumewasiliana na TCRA kufuatia maelekezo ya Waziri Nape kuhusu malalamiko hayo ya wateja.

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger