Ticker

6/recent/ticker-posts

We Acha Kabisa Kwa Yanga Hii Hakuna Cha Simba Wala nini Wamtungua Dodoma Jiji Viwili Bila...VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga wamekamilisha dk 45 za mwanzo wakiwa mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji, kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.

Kasi ilianza ndani ya dakika 10 za mwanzo ambapo presha ilikuwa kubwa na Yanga ikapachika bao la kuongoza dk ya 11 kupitia kwa Dickosn Ambundo.

Winga huyo ambaye alisajiliwa Yanga akitokea ndani ya Dodoma Jiji ilimpasa awaombe msamaha mabosi wake hao wa zamani.


Katika harakati za kuokoa shuti la Zawadi Mauya kipa wa Dodoma Jiji pigo la kwanza alifanikiwa kulitoa alipojaribu mara ya pili akajifunga ilikuwa dk ya 35.


Ni Mohamed Yusuph ambaye aliweza kujifunga na kuwafanya Dodoma Jiji kukamilisha dk 45 wakiwa wametunguliwa mabao 2-0.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments