Yanga, Ruvu Mwisho wa Reli leoVINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga leo watahitaji ushindi wa aina yoyote dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma ili kufikisha pointi 58 zitakazowafanya kuingia sebuleni mwa chumba kilichohifadhiwa kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wakati Yanga ikihitaji ushindi huo, Ruvu Shooting nayo ambayo imeupeleka mchezo huo mjini Kigoma, itakuwa inahitaji ushindi kwa hali yoyote ile ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kubaki Ligi Kuu msimu ujao.

Klabu ya Yanga imesema inauhitaji ushindi huo si tu kuukaribia ubingwa, lakini kuwapa wanachama na mashabiki wake zawadi ya sikukuu ya Idd El Fitri, huku Ruvu Shooting ikidai kama Kigoma ni mwisho wa reli, basi leo ndiyo itakuwa mwisho wa Yanga kutopoteza mechi yoyote ile.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, amesema timu yao imepata mapokezi makubwa na mazuri, hivyo cha kuwalipa ni ushindi.

"Tumefika salama na tumepata mapokezi makubwa, kwani mara ya mwisho kutuona mashabiki wa Kigoma ni kwenye fainali za Kombe la FA msimu uliopita, lakini hawakupata bahati ya kuwaona kina Fiston Mayele, Khalid Aucho na wengine na hii ilikuwa ni fursa yao kuwaona. Tumekuja kukusanya pointi tatu, tunaiombea timu yetu ipate matokeo mazuri ili tuwape wanachama na mashabiki wa timu hiyo Idd Mubarak," alisema Bumbuli.


Akizungumzia adhabu ya faini ya shilingi milioni tatu waliopigwa na Bodi ya Ligi alisema hiyo wameiona na kwa sababu fedha zao za mechi yao dhidi ya Simba zimeingia hawana wasiwasi.

"Mlango ambao tuliingilia kwenye Uwanja wa Azam Complex msimu uliopita, ndiyo huo huo tuliingilia, adhabu tumeiona, fedha zetu za mechi dhidi ya Simba zimeshaingia, tutalipa na mambo mengine yanaendelea, sisi tunatafuta ubingwa, timu ipo Kigoma, tupo vizuri," alisema.

Yanga ni moja kati ya timu iliyotozwa faini na moja kati ya kosa ni kuingia kwenye mlango usio rasmi kwenye mechi yao dhidi ya Azam FC iliyofanyika kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Aprili 6 na kushinda mabao 2-1.

Naye msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema leo ndiyo itakuwa mwisho wa Yanga kucheza mechi bila kupoteza.

"Kwa sababu Kigoma ni mwisho wa reli, sasa tunataka iwe mwisho kwao kuendelea kutopoteza. Tumejizatiti, tuko vizuri na tuko tayari.

Ruvu Shooting inakamata nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi, ikiwa na pointi 21 hadi sasa.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad