Ticker

6/recent/ticker-posts

Yanga Wameona Isiwe Tabu Wampa Kibwana Shomari Mkataba Mpya Hadi 2024

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA


Hatimaye Uongozi wa Young Africans umekamilisha mpango wa kumsainisha mkataba mpya Beki wa Kulia Shomari Kibwana, na kuzima maneno yaliyochukua nafasi kwenye mitandao ya kijamii kwa kudai mchezaji huyo alikua mbioni kuachwa.


Kibwana Shomari amesaini mkataba mpya wa miaka miwili ambao utamuwezesha kuendelea kukipiga Young Africans hadi Juni 2024.


Baada yakukamilisha taratibu za kusaini mkataba huo Kibwana alizungumza na Mashabiki wa Young Africans kupitia Video fupi iliyowekwa kweye kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo, akisisitiza kuwa anaamini jambo hilo limewafurahisha.


“Wananchi leo ninayo habari ya kutangaza, wapo watakaoipenda na wasioipenda, kama hujaipenda usitazame, ninaendelea kubaki Yanga kwa miaka miwili.” Amesema Kibwana.


Kibwana alisajiliwa Young Africans mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Mtibwa Sugar, na hadi sasa ameonyesha kuwa muhimili mkubwa katika safu ya ulinzi ya klabu hiyo, akicheza upande wa kulia na kushoto pale anapohitajika kufanya hivyo

Post a Comment

0 Comments