5/29/2022

Zamaradi "Sina hofu na maisha yangu"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Mtangazaji na mjasiriamali maarufu nchini Zamaradi Mketema afunguka kwa undani siri za chanzo cha kuchukua uamuzi wa kuyaweka mahusiano yake ya kimapenzi hadharani kupitia kwenye mitandao ya kijamii.

Jambo ambalo limekuwa likitazamwa kwa taswira ya tofauti huku baadhi ya watu wakiwamo mashabiki wake wahidhihirisha kuhofia hatma ya mahusiano hayo kutokana na kukithiri kwake kuyanadi bila hofu.

Akizunguma na Dar24Media Zamaradi amebainisha kutokuwa na shaka juu yeye kuzungumziwa vibaya, huku akisisitiza kwamba suala la kuyaweka maisha ya familia yake wazi kwenye mitandao halijatokea kwa bahati mbaya bali ni umauzi wake binafsi wenye kufanya aishinkwa furaha..

“Mimi namuamini sana Mungu, kitu chochote nilichonacho ni Mungu, sina nguvu ya kulinda kitu ambacho Mungu amepanga kiondoke, na sina tabia ambayo inaweza kupoteza kitu ambapo Mungu amepanga kikae, kwa hiyo sina hofu.


Sina hofu kwa sababu namuamini Mungu, vyovyote nilivyo ni Mungu, siri yangu moja kubwa siishi kwa wasi wasi, najiamini sana na ni kwasababu nina muamini sana Mungu.

So kuishi maisha ya wazi kimahusiano, ni mume wangu, ninampenda ananipenda, hii nasema kwa uhakika ananipenda’ na nina furaha” amesema Zamaradi.

Aidha Zamaradi amedokeza kuwapo kwa baadhi ya watu wake wa karibu ambao wamekuwa na hofu kuhusu kudumu kwa ndoa yake kutoka na mfumo wa maisha aliouchagua. “Kuna rafiki yangu mmoja aliwahi kunipigia akaniambia unajiamini nini kuishi hivyo?, unajiamini nini kumposti? kuna watu.


Nikamwambia kuna watu wanaishi na waume zao wamewaficha lakini wanapigana kila siku, kumuweka mpenzi wako wazi na kumficha, yaweza kuwa ni uamuzi sawa, kila mtu yuko sahihi ilimradi kiwe ni chenye kukupa furaha” ameongeza.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger