5/07/2022

Zuchu Aiandikia Basata na TCRA Barua ya Wazi...Rosa Ree na Video yake ya I'm Not Sorry Yatajwa

Nafasi za Ajira Jiunge Group la Telegram la AJIRA YAKO Kwa Kubonyeza >> HAPANi matumanini yangu mpaka sasa kila mtu anafahamu kua Video Ya wimbo wetu pendwa “MTASUBIRI “ Umesitishwa kuonekana kwenye vyombo vya habari Nchini kwetu .Nimeona bora nianze moja kwa moja kwenye mada husika .Jana Nilipokea taarifa hizi kupitia mitandao kama Nyinyi tu mashabiki zetu kwamba wimbo wetu unapigwa marufuku sababu tajwa kua inaleta ukakasi kwenye jamii husika mwisho wa kununukuu .

Awali ya yote niseme kama msanii nilietumia ubunifu kukaa chini na muongozaji wa video yetu takribani siku 4 kuunda stori ambayo kwa utashi wangu na heshima niliyonayo kwa dini zote na madhehebu yake sikuona huu ukakasi unaoongelewa hapa.Nafahamu si kila kazi ya kisanaa itamfurahisha kila mtu lakini kuvunjia heshima dini si kitu ambacho kipo ndani ya weledi wa kazi yetu sababu tunafahamu fika tunao mashabiki wa dini zote na kulinda hisia zao ni moja ya nguzo kuu Kwenye mziki hatueki matabaka .Ifahamike kwamba mimi ndie nilishoot hiyo scene ikinitaka kuwepo kanisani nikiwa nafanya mazoezi ya kwaya sio misa ni mazoezi ya kikwaya nikiwa nimevalia joho lenye stara .Kanisa hili lipo kisarawe na kabla ya kushoot masister walitukagua na kusikiliza kwa makini stori yetu na kuridhishwa nayo ndipo hapo tukapewa ruhusa ya kushoot .Naomba nielekeze malalamiko yangu kwa mamlaka husika BASATA walezi na wazazi nimeambatanisha video na movie baadhi ambazo zimetoka kabla ya mtasubiri vipi hizi hazina ukakasi
 .Lakini ni jamii ipi hiyo iliyoleta malalamiko mpaka nyie kufungia video iliyogharimu muda wa siku nne na pesa nyingi kuishoot tena mkaifungia bila hata kutaka kusikiliza utetezi .
Mtasubiri video ni ya kawaida sana A very innocent sweet story .Naumia sababu hii inaenda kudumaza sio tu mziki ila Tasnia nzima kwa ujumla .HAYATI baba wa taifa alisema “Utii ukizidi huzaa uoga ,Uoga huzaa unafiki na kujipendekeza mwisho wake Umauti “
Huu ndio umauti wa Tasnia hii unapoanzia
INAENDELEAA
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger