5/09/2022

Zuchu: Mirabaha Wasanii wa Wcb Hatukunusa Top List Wakati kitwakwimu tunaongoza


Huu ndio umauti wa Tasnia hii unapoanzia .Sijui nileleze vipi hisia zangu zipokelewe kwa heshima ya kutosha na utii bila ya kuchukuliwa kama mjeuri ila kwa hili mumetuonea .

Sisi ni vijana tunaotafuta rizki bila ya kuchoka lakini pengine Wazazi wetu @basata.tanzania mmekua mstari wa mbele kutuvunja nguvu mbele ya jamii bila kujali hisia muda vipaji na uwekezaji unaofanyika .Hapo awali mlitoa mirabaha Wasanii wa Wcb Hatukunusa Top List Wakati kitwakwimu za namba ,MAUZO na ufanyaji vizuri Katika Chati zote Kasoro yenu nyinyi @basata.tanzania @cosotatanzania Nini shida wazazi wetu .Inawezekana vipi .

Kisha hapo Tunalaumiwa kwa kutoshiriki Tuzo .Ni wazi kua Hii imekua wazi sasa kama mamlaka ya kisanaa inafanya kazi Kupinga juhudi za WCB lakini pengine hii hasira mnayoipandikiza juu yetu tunaihitaji kwa mafanikio chanya yetu na mashabiki zetu wanaotupigania .mwisho niseme kazi iendelee Mashabiki zetu ,Maboss zetu mtusamahe sana kwa kero mnayokutana nayo haiko mikononi mwetu Wenye mamlaka washasema sisi ni nani? tuwe na subra na msituache mana nyinyi ndo kimbilio letu la mwisho Nawapenda sana .Sikukuu njema KAZI IENDELEE

HABARI HIZI ZA UDAKU ZINAPATIKANA KATIKA APP YA UDAKU SPECIAL, IDOWNLOAD>> HAPA BURE 

Share:
Loading...

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger