6/02/2022

Amuua binti wa miaka 7, baada ya kumnajisi

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


POLISI mkoani Pwani wanamsaka mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa, mwenye umri kati ya miaka (30) na (40) kwa tuhuma za kumnajisi na kumua kwa kumziba na chandarua mdomoni mwanafunzi wa darasa la pili mwenye umri wa miaka (7), aliyekuwa anayesoma shule ya Msingi Misugusugu.

Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani, Pius Lutumo, mtuhumiwa alitendea tukio hilo nyumbani kwake, Mei 30 mwaka huu Mtaa wa Vitendo Misugusugu, Kata ya Misugusugu wilayani Kibaha, ambapo baada ya tukio hilo mtuhumiwa alitoroka.

 "Uchunguzi wa awali umebaini mtuhumiwa alifanya tukio hilo la mauaji, wakati akimbaka mwanafunzi huyo, ambapo alimziba mdomo kwa kutumia chandarua, ili asipige kelele huku akimbaka na kusababisha kifo hicho," amesema Lutumo.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger