6/13/2022

Anerlisa Aanza Kufunguka Taratibu "Mwanaume Niliyekuwa Naye Kwenye Mahusiano Alitaka Kunitapeli Milioni 70"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


 Anerlisa mrembo tajiri toka nchini Kenya alipoulizwa ameeleza sababu za mahusiano yake na wanaume aliowahi kuwa nao kuvunjika. amesema mmoja wa ma ex wake alitaka ampe namba yake ya siri ya kadi ya ATM 😲 lakini hakuthubutu


Pia mmoja wa wanaume aliyewahi kuwa nae katika mahusiano siku moja alimwambia mrembo huyo kuwa tumekaa pamoja zaidi ya mwaka katika mahusiano ni kwanini usinijengee nyumba au kunifungulia kampuni kama yako😲


Anerlisa alimjibu kuwa hilo sio lengo la yeye kuwa katika mahusiano na mwanaume, amesema haikuchukua wiki aliachwa na mwanaume huyo


Pia ameshauri kinadada usiwe kwenye mahusiano na mtu msiri sana, amesema yeye kuna siku alifika alipokuwa mmoja wa ex wake bila ex wake huyo kujua, alipofika alimsikia mwanaume husika akiwa na mwenzake wanamuongelea yeye Anerlisa, mwanaume husika akieleza kutaka kumtapeli mrembo huyo dola $30,000(Tsh.70.4 milioni). Mahusiano yao yakaisha


Anerlisa anayemiliki kampuni yenye mafanikio, amesema kuwa yeye huwa hatoi pesa kwa mwanaume isipokuwa ataonesha moyo wa upendo kwa mwanaume lakini si kuja kuliwa pesa zake


Amesema huwa anaishia kucheka akisikia watu wakimsema mwanaume huyu au yule kuwa aliwahi kuwa katika mahusiano na Anerlisa ila hajaambulia chochote na ni kwasababu yeye sio mtu wa kulea mwanaume


Hata hivyo, mrembo huyo ambaye wazazi wake pia wanajiweza hakutaja jina la ex wake yeyote yule hivyo hali kubaki tete mashabiki kuumiza kichwa kujua japo jina la ex husika

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger