6/12/2022

Anerlisa Afunguka "Ex Aligoma Kufunguliwa Biashara, Alitaka Pin Yangu ya ATM"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Anerlisa amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki wa Tanzania Ben Pol

ANERLISA Muigai; ni mrembo mwenye pesa zake wa nchini Kenya na ex wa staa wa muziki wa RnB nchini Tanzania, Ben Pol ambaye anasema kuwa, kuna ex-wake mmoja (hajasema kama ni Ben Pol) alitaka amfungulie biashara, jambo ambalo alilikataa na huo ukawa mwisho wa penzi lao.

Mrembo anasema kuwa, suala la kuomba pesa kila wakati katika mapenzi ni kitu ambacho alikuja kubaini kuwa watu wanaenda kwake kwa ajili kujinufaisha na siyo mapenzi.

Anerlisa mwanamama mjasiriamali raia wa Kenya

“Nilikuwa kwenye mahusiano ambapo mwenzi wangu alianza kuniambia nimwambie pin ya ATM, wakati mwingine nikiongea na mama yangu anataka kujihusisha na mazungumzo yetu.

“Wacha nicheke, mmoja wa ma-ex wangu aliniuliza tumekuwa pamoja kwa mwaka mmoja kwa nini nisimsaidie kama vile kumjengea nyumba na hata kumfungulia kampuni kama yangu, nilimjibu nikamwambia kama uliona kuanzisha uhusiano na mimi kutakutajirisha haya basi uko kwenye uhusiano ambao haufai,” anasema Anerlisa.


Anerlisa aliwahi kuolewa na Ben Pol, lakini ndoa yao ikadumu kwa muda mfupi.


Katika mapenzi yao, mrembo huyo alitokea kwenye video ya wimbo wa Ben Pol wa Kidani kama video vixen.

Cc; @sifaelpaul

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger