Askofu ataka kusomwa dua kuwafichua wauaji wa mapadri
 
Askofu ataka kusomwa dua kuwafichua wauaji wa mapadri
MWENYEKITI wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Mashehe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini, Askofu William Mwamalanga amewaomba mapadri nchini kufanya dua maalumu kwa ajili ya kuwafichua wauaji wa mapadri wawili wa Kanisa Katoliki wa  Shirika la Wamisionari wa Afrika (White Fathers).

Mapadri hao waliouawa kwa nyakati tofauti ni Michael Samson wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya aliyetenganishwa kichwa na kiwiliwili na mwili wake kukutwa pembeni ya Mto Meta mkoani humo na Francis Kangwa wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri aliyekutwa amekufa ndani ya tangi la maji.

“Tufanye dua maalumu kwa ajili ya waliodhamiria mabaya kwa mapadri wa White Fathers, tutumie umoja wetu na wananchi kwenye mikoa ya Dar es Salaam na Mbeya hadi tugundue chanzo cha ukatili huo.”

“Tunaungana na wakazi wa Jiji la Mbeya  na Wakatoliki wote nchini kuyalaani mauaji hayo ya kikatili na tunamuomba Mungu atusaidie kuwafichua wauaji hao popote walipo ambao ni dhahiri wamekusudia jambo baya kwa mapadre wa shirika hilo nchini,” alisema.

Askofu Mwamalanga alisema maaskofu wanaungana na Jeshi la Polisi kuwaomba wakazi wa Mbeya na Dar es Salaam kutoa ushirikiano mkubwa kwa jeshi hilo ili kuwafikia wauaji hao. 

Aidha, amekemea vitendo vya baadhi ya watu kujichukulia sheria mikononi na kuwataka kuvitumia vyombo vya sheria.
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad