Ticker

6/recent/ticker-posts

Bernad Morrison Afunguka A to Z Sakata Lake na Timu ya Simba 'Nilikataa Kusign Mkataba Mpya"


Kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ghana, Bernard Morrison amefanya mahojiano maalum na kituo cha Global Tv kuhusiana na masuala mbalimbali yanayomuhusu ikiwemo sababu za kuondoka Simba na klabu anayoelekea.


Kwenye mahojiano hayo Morrison amefunguka mambo mengi nyuma ya pazia ambayo yalikuwa yakiendelea alipokuwa Simba.


“Walinipa mapumziko maana nilikataa kusaini mkataba mpya, kama ningecheza Simba miaka 5 au 10 alafu mwisho wa siku nikarudi Ghana sina hela au kumpgia mwenyekiti naomba hela kuisaidia familia yangu sio kitu kizuri”


“Niliomba mkataba mzuri, maboresho kwenye mkataba ili niwe vizuri kuihudumia klabu na haikufanyika hivyo, nilikuwa na kikao na Barbara na sababu Ya hicho kikao ni kwa sababu tulicheza mechi dhidi ya Yanga na ile mechi nilipata majeraha na awali tayari nilikuwa majeruhi kwenye mechi dhidi ya Orlando Pirates”


“Baada ya mechi daktari hakunifuata kunihudumia wala kujua hali yangu, nilimtumia meseji nyingi kuwa sipo sawa lakini hakufanya hivyo, niliwaambia hamnijali hivyo nililazimika kujihudumia mwenyewe nikiwa nyumbani. CEO alinipigia simu nikaenda ofisini kwake akaniambia wachezaji wanahasira, wanasema hawataki niende tena kambini wala mazoezini, kocha analalamika siwaheshimu, hawataki niende mazoezini hivyo malalamiko ni mengi ni kwa nini nafanya hivyo ?”


“Nilimjibu sio kweli sidhani kama wachezaji wanaweza kufanya hivyo maana ndio hao hao wachezaji wananipigia simu nisipoonekana kambini kunijulia hali lakini wewe CEO unasema hivi, Bocco, Mkude, Chama, Bwalya walikuwa wananijulia hali kila siku,” - Ameeleza Bernard Morrison.

Nafasi za Ajira Jiunge na Ajira Yako Telegram Group

 CLICK HERE


Post a Comment

0 Comments