6/20/2022

Rais Biden Aanguka na Baskeli Mbele ya Wanahabari

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Rais wa Marekani Joe Biden aliripotiwa kuanguka kutoka kwenye baiskeli yake karibu na nyumba yake ya Rehoboth katika ufuo wa Delaware mnamo Jumamosi Juni 18, 2022 muda mfupi baada ya kusalimia waandishi wa habari kwa kuwapungia mkono.


Rais huyo mwenye umri wa miaka 79, akiwa ameambatana na maafisa wa usalama wa ‘Secret Service’, alikuwa akisafiri kwa mwendo wa kasi kwa mazoezi kabla ya kufunga breki ili kuzungumza na umati wa watu uliomtakia “Siku Njema ya Akina Baba” kisha akateleza.

Kwa mujibu wa tarifa kutoka shirika la habari la Foxnews, Biden amekuwa akionekana mara kwa mara akifanya mazoezi na baiskeli yake kuzunguka maeneo ya karibu na nyumba yake na anatema alikua akitaka kusi mama ambao muu wake ulikamatwa na Pedali ya baiskeli na kujikuta akianguka kabla hajafanikiwa kuushusha.

Hata hivyo, alipoulizwa na waandishi wa habari kama yupo sawa, Biden alijibu “nipo sawa kabisa na sina haja ya kuhitaji msaada wa kimatibabu.”Wakati tukio hilo linatokea mke wake, Jill Biden, tayari alikuwa amepiga kona na kukosa kushuhudia mumewe akianguka.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger