Ticker

6/recent/ticker-posts

Diamond Platnumz Ampongeza Manara, Young Africans Kwa Ubingwa

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA

 


Mwanamuziki Nguli wa Tanzania Nassibu Abdul ‘Diamond Platinum’ amempongeza Msemaji wa Young Africans Haji Sunday Manara, kufuatia Klabu ya Young Africans kutwaa Ubingwa wa 28 wa Tanzania Bara jana Jumatano (Juni 15).


Young Africans ilijihakikishia kuwa Bingwa wa Tanzania Bara, baada ya kunyakua alama tatu za mchezo wake na Coastal Union uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0.


Diamond amempongeza Manara ambaye alijiunga na Young Africans mwanzoni mwa msimu huu 2021/22 akitokea Simba SC, kwa sababu zilizotajwa kutokua na maelewano mazuri na Afisa Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez.

Katika Ujumbe wa Diamond amethibitisha kufahamu madhila aliyopitia Haji Manara kabla ya kuondoka Simba SC, huku akiandika MUNGU wetu ni MKUBWA KULIKO FITNA ZA BINADAMU.

Diamond ameandika: “MUNGU WETU ANA NGUVU KULIKO FITNA…. Super proud of you my brother Haji Manara na YOUNG AFRICANS NZIMA”

“Kiukweli kama kijana ninayepambana kujikwamua na umaskini leo nilipanga niongee vitu vingi sana ambavyo watu wasingevitegemea…..”

“…. Kwa sababu mimi ni miongoni mwa watu waliojua kuhusu sakata lako (Haji) mpaka leo kuwa Yanga, pengine kuliko wengi”

“Ila acha tu niishie kusema MUNGU wetu ni MKUBWA KULIKO FITNA ZA BINADAMU 🏆”

🔍 Diamond Plutnumz CEO Wasafi Media

Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Tanzania Zipo HAPA

Ufadhili wa Masomo ( Scholaships) Bonyeza HAPA

Post a Comment

0 Comments