6/17/2022

Dulla Makabila Acharuka 'Mwambieni Nay wa Mitego Simuogopi Naweza Kumvunjia Heshima Muda Wowote"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Dulla Makabila amemjibu Nay wa Mitego baada ya Rapa huyo kutumia ukurasa wake wa Instagram upande wa Insta story na kuandika kuwa ukiacha wachache, idadi kubwa ya waimbaji wa Singeli hawajielewi, akimtolea mfano Dullah makabila kuwa ni moja ya ambao hawajielewi,kichwani ni Zero. Hii inakuja baada ya msanii Makabila kuandika walaka mrefu sana wa kuomba radhi kwa msanii Diamond Platnumz.


Hasa kupitia Empire ya EFM hii leo June 16, Dullah amedai Nay ni brother wake lakini anapaswa kujua kuwa anamuheshimu na sio kuwa anamuogopa, hivyo anaweza mvunjia heshima muda wowote ule, kama angekuwa na busara basi angemfwata private kumwambia amekosea na sio kwenda kumtukana hadharani. Makabila pia amemtaka Nay wa Mitego amuombe msamaha haraka.


Dullah anaamini hakuna baya alilofanya na wanao ona amekosea wana chuki binafsi na Diamond.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger