6/15/2022

Esma Platnumz 'Mama Dangote Ndio Rafiki Yangu Pekee wa Ukweli"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Esma Khan  au Esma Platnumz; ni mwanamama maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) na mjasiriamali nchini Tanzania ambaye anasema kuwa, mama yake, Sandra Kassim @mama_dangote almaarufu Mama Dangote ndiye rafiki yake pekee.

Esma ambaye ni dada wa staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz anasema hiyo ndiyo sababu amekuwa akionekana naye mara nyingi.

Esma anasema kuwa, Mama Dangote siyo mzazi tu, bali ndiye rafiki yake mkubwa.

“Yeye (Mama Dangote) ndiye rafiki yangu pekee aliyekuwepo. Mimi sinanga marafiki. Marafiki wengine huja na mambo yao,” anasema Esma.

Esma anasema alimchagua Mama Dangote kuwa rafiki yake kwa kuwa huwa anamsapoti katika kazi yake (biashara ya vitambaa) kwa dhati.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger