6/17/2022

Flora Mvungi Amcha Vibaya H Baba "Unajiita Baba Huku Wanao Wanalelewa Ukweni"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Mwigizaji wa filamu na mwimbaji nchini, msanii Florah Mvungi ametumia ukurasa wake wa Instagram kutupa jiwe gizani kwa maneno pambe akiwalenga wababa wenye tabia ya kuwatelekeza watoto wao ukweni, akiwaambia kwamba "Baba" sio jina la ubatizo wapambane.


Hata hivyo ujumbe huo umepokelea kwa maoni tofauti huku ikidhaniwa ni ujumbe mahususi unaomlenga mzazi mwenzake ambaye ni mwanamuziki H.Baba.


"Unajiita baba halafu wanao wanalelewa ukweni ๐Ÿ˜pambana wewe! Baba sio jina la ubatizo mfyuuu. Watoto wanatembea na baraka zenu wababa, mnaweza mkawa mnapata mikosi kila siku kumbe laana za watoto ๐Ÿ‘Œ๐Ÿ‘Œ. Usitafute mchawi wala hujalogwa, tengeneza na Mungu kwanza," - Unasomeka ujumbe wa @florahmvungiofficial1 kupitia ukurasa wake wa Instagram.


Ikumbukwe, Florah na H.Baba pamoja wana watoto wawili ambapo Florah na wanae makazi yao ni jijini Dar es salaam huku H.Baba akiishi jijini Mwanza.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger