Habari Njema Unafuu bei Mafuta ya Kula waja

 


Serikali imesema inapendekeza tozo ya asilimia sifuri katika bidhaa za mafuta ya kula yanayozalishwa nchini kwa mwaka mmoja, ili kuleta unafuu wa bei kwa bidhaa hiyo, sambamba na kutoa msamaha wa VAT kwenye miti ambayo haijachakatwa.


Hayo yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba Bungeni jijini

Dodoma wakati akisoma hotuba ya mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya

serikali kwa mwaka wa fedha 2022/23.


Amesema pia Serikali inapendekeza kutoza VAT kwa kiwango cha sifuri kwenye mbolea inayozalishwa

nchini kwa mwaka mmoja, kutoa VAT kwenye vifaa vya kupima kiwango cha maji na

unyevunyevu kwenye udongo.


“Kutoza VAT kwa kiwango cha sifuri kwenye mbolea inayozalishwa nchini kwa mwaka mmoja, kutoa VAT kwenye vifaa vya kupima kiwango cha maji na unyevunyevu kwenye udongo itapunguza mapato ya serikali ya Sh. bilioni 2.99,” alisema.


Waziri Mwigulu pia alipendekeza kusamehe VAT kwenye magari yenye jokofu na vyumba vya ubaridi ili

kuzuia mazao kuharibika baada ya mavuno na kuchochea kilimo cha kisasa, huku akipendekeza kuondoa msamaha wa kukata Kodi ya Zuio kwenye malipo ya upangishaji nyumba.


“Kuondoa msamaha wa kukata kodi ya zuio kwenye malipo ya upangishaji nyumba na majengo ya biashara na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato (TRA) ataingia makubaliano ya uwakala na Ofisi ya Rais – TAMISEMI juu ya usimamizi na ukusanyaji wa kodi hiyo” aliongeza.


Aidha, Waziri huyo pia alipendekeza kuanzisha utaratibu wa kutoza ada ya Sh. 1,000 hadi 3,000 kwenye ada ya matumizi ya king’amuzi kulingana na kiwango cha matumizi, na kuongezakuwa kuanzia mwaka ujao wa fedha, kiongozi wa serikali pindi wanapotumbuliwa na kupangiwa majumu mengine, watalipwa mishara yao kwa viwango vya zamani.


“Napendekeza yeyote aliyetokea kwenye nafasi yake ya kuteuliwa akitolewa na

akabaki kwenye utumishi wa umma arejee pia kwenye mshahara wake wa zamani ili

kuwapunguzia Watanzania mzigo wa kuwalipa watu waliokaa benchi huku wakiziba nafasi za

vijana wapya kuajiriwa,” alisema.


Kuhusu mkakati wa kubana matumizi, amesema Serikali inatarajia kudhibiti mambo kadhaa ikiwemo ununuzi na matumizi ya magari kwa kuzingatia waraka wa Rais namba moja wa mwaka 1998 kuhusu hatua za kubana matumizi ya serikali.


“Pia tutazingatia waraka wa Mkuu wa utumishi wa umma namba mbili wa mwaka 2021 kuhusu utaratibu wa kutumia usafiri huo, baadhi ya maeneo yenye gharama kubwa kwa serikali ni ununuzi wa magari, mafuta ya uendeshaji, vipuri na matengenezo,” alifafanua Waziri Mwigulu

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad