6/15/2022

Hali Tete Bwana Harusi Akimpiga Bi Harusi Wakati wa Harusi yao

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Mwanamume huyo anadaiwa kula mori baada ya bibi harusi wake alipomshinda kwenye mchezo wakati wa tafrija ya harusi yao
Bibi harusi alishinda mchezo huo, na bwana harusi alipogundua kuwa ameshindwa, alimpiga kwa nguvu nyuma ya kichwa
Huku akipuuza matendo yake, bwana harusi alisimama jukwaani, akiangalia umati wa watu waliokuwa kimya
Video ya bwana harusi akimpiga bibi harusi wake kwenye harusi yao imeibua hasira kwenye mitandao ya kijamii.

Bwana harusi alipogundua kuwa ameshindwa, alimpiga kwa nguvu nyuma ya kichwa
Bwana harusi alimpiga kwa nguvu bibi harusi nyuma ya kichwa wakati wa tafrija ya karamu yao. Picha: Skrinishoti kutoka kwenye video.
Mwanamume huyo anadaiwa kula mori baada ya bibi harusi wake alipomshinda kwenye mchezo wakati wa tafrija ya harusi yao.

Wanandoa hao walikuwa jukwaani wakati wa tafrija ya harusi yao, ambayo ilifanyika nchini Uzbekistan, wakati msimamizi wa karamu hiyo alipowafanya washiriki katika shindano.

Bibi harusi alishinda mchezo huo, na bwana harusi alipogundua kuwa ameshindwa, alimpiga kwa nguvu nyuma ya kichwa kwa mkono wake.


 
Mwanamke Aliyenaswa kwenye Kamera Akitishia Kuwakamata Watu Kilabuni Sio Polisi
Akiwa amestaajabishwa, bi harusi aliweka mkono wake kichwani, kabla ya kunyanyua nguo yake nyeupe ya harusi kutoka sakafuni na kuongozwa kutoka jukwaani na wanawake wengine wawili.

Huku akipuuza matendo yake, bwana harusi alisimama jukwaani, akiangalia umati wa watu waliokuwa kimya ambao walikuwa wakishangilia kwa sekunde chache zilizopita.


HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger