Hamisa Aunguka “Endeleeni Kubana Pua Mkinisema Vibaya Mapambano Yanaendelea!”

 


HAMISA Hassan Mobeto; ni mmoja wa wanawake warembo na mastaa nchini Tanzania. Wiki iliyopita, mbali na Kajala Masanja kukubali kumrudia Harmonize kuzungumzwa zaidi, lakini mwingine aliyeongoza kuzungumzwa ni mwanamama Hamisa.


Hamisa amezungumzwa kwa mambo mawili; kwanza ni kitendo cha kuachia rasmi albam fupi (EP) yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wake.


EP hiyo inakwenda kwa jina la Yours Truly na ina jumla ya ngoma 4 na bonus track moja ambapo amewashirikisha wakali kama Otile Brown wa Kenya na Korede Bello wa Nigeria.


 


Yours Truly ni EP ya kwanza kwa Hamisa tangu aanze safari yake ya muziki na inapatikana exclusive kupitia mitandao yote ya kupakua na kusikiliza muziki duniani.


Pili; Hamisa amezungumzwa kutokana na ukaribu wake na rapa mkubwa duniani wa Marekani, Rick Ross ambaye alifanya naye mazungumzo ya moja kwa moja kupitia Insta Live na jamaa huyo akaeleza anavyomzimia mwanamama huyo na mipango yake kedekede ambayo wengi wanasema ameupiga mwingi.


Kupitia safu hii ngoja tuiangazie safari ya ustaa ya Hamisa hadi hapo alipofikia utakuwa na la kujifunza.


Awali kabisa, Hamisa alizoeleka kutumiwa na wasanii kwa video zao kama video vixen, lakini sasa ni  mwanamitindo, mwanamziki, muigizaji na mfanyabiashara.


Si ajabu sasa kumuona Hamisa akitumiwa na kampuni kadhaa katika matangazo ya biashara. Pia anamiliki kampuni yake mwenyewe kwa jina Mobetto Styles.


Ukihesababu wanawake ambao wamewahi kutoka kimapenzi na staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz, huwezi kukosa kumtaja Hamisa.


Hamisa na Diamond walikuwa wapenzi na wakajaaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Dyllan.


Hamisa amezaliwa Desemba 10, 1994 huko jijini Mwanza nchini Tanzania. Kwa sasa ana umri wa miaka 28 na siyo 25 kama baadhi ya watu wanavyomkejeli kwamba miaka yote umri wake ni huohuo na huwa haubadiliki.


Hamisa alisomea Shule ya Msingi ya Mabatini, Mwanza kisha akaja kumalizia jijini Dar na kujiunga na Sekondari ya Tandika na akaishia kidato cha nne, lakini anazungumza Kingereza kilichonyooka cha Kimarekani.


Kama nilivyodokeza kwenye utangulizi, Hamisa ni mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania akibebwa na umbo lake lavutia ndiyo sababu hutumiwa na kampuni nyingi kwa ajili ya matangazo kwani kampuni zenyewe zinafahamu kuwa akifanya matangazo yatawafikia wengi kutokana na wingi wa wafuasi zaidi ya milioni 9 wa kwenye Instagram pekee.


Pia kutokana na mvuto huo aliuza sura kwenye video kibao kama Baby ya Quick Racka na Ngwair, Salome ya Diamond, Dodo ya King Kiba na nyinginezo.Kwenye muziki wengi walimsema Hamisa kuwa hajui kuimba, lakini amesikika na ngoma nyingi kama Madam Hero, Sensema, My Love, Ginger Me, Boss, Sawa na sasa anakiwasha kinoma na EP yake ya Yours Truly.

Kwenye familia, Hamisa amebarikiwa na watoto wawili. Msichana na mvulana.


Mtoto wa kwanza anajulikana kama Fantasy mwenye umri wa miaka saba na Dyllan ambaye ana miaka minne.


Amemzaa Fantasy na CEO wa EFM na ETV, Dj Majizzo na Dyllan amezaa na Diamond ambaye mwanzo alimkataa na ikabidi vipimo vya DNA vifanyike.

ya majibu kuonesha wazi kwamba mtoto yule ni wa Diamond ndipo jamaa alimkubali. Wakati mtoto huyo anazaliwa, Diamond alikuwa kwenye uhusiano na Zari The Boss Lady. Hiyo ndiyo sababu iliyowafanya wawili hao kuachana.


Hamisa anasukuma ndinga kali aina ya Land Cruiser Prado ambalo amenunua kwa pesa zake mwenyewe huku akiishi kwenye mjengo wa kifahari huko Mbezi- Beach jijini Dar.


Utajiri wa Hamisa unakadiriwa kufikia Dola za Kimarekani milioni 1 (zaidi ya shilingi bilioni 2 za Kitanzania).


Utajiri wa Hamisa unatokana na kampuni yake ya mavavi ya Mobeto Styles, matangazo ya biashara, kutumika kama video vixen, mauzo ya muziki na madili mengine kwani mwenyewe anasema ni mwanamke mchakarikaji.


Huyu ndiye Hamisa; ambaye baadhi ya wadada wa mjini wasio na kazi za kufanya zaidi ya kushinda kwenye Instagram huku wakibana pua na kumsema vibaya kwa kila analolifanya, lakini yeye anasema waendelee kubana pua yeye ni aluta continua na mapambano yanaendelea!

______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad