Harmonize na Anjella Wapigwa na Kitu Kizito na Mabosi wa Nandy, Ngoma Yao Yapigwa Chini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 


ANJELLA na bosi wake, Harmonize wamepigwa na kitu kizito baada ya video yao mpya inayokwenda kwa jina la Kioo kuondolewa kwenye mtandao wa YouTube kutokana na malalamiko ya hakimiliki (copyright claims) kutoka Kampuni ya Mr Eazi ya Empawa Africa ambayo ndio wanasimamia usambazaji wa Nyimbo za Nandy


Hayo yanajiri baada ya Januari 2020 video ya wimbo wa msanii kutoka Konde Gang, Killy unaokwenda kwa jina la Ni Wewe ambao amemshirikisha Harmoninze nao kuondolewa YouTube kutokana na malalamiko ya hakimiliki (copyrighty claims) kutoka kwa mtu anayetambulika kwa jina la Mutisya Munyithya kutoka Kenya.


Juni 2021, Wimbo wa Harmonize wa Sandakalawe nao uliondolewa YouTube kutokana na masuala ya hakimiliki baada ya kampuni ya usambazaji muziki ya Empire kulalamika kuwa wimbo huo umechukua baadhi ya vionjo kutoka kwao.


Kabla ya hapo, Agosti 2020, wimbo mwingine wa Harmonize wa Ameen uliondolewa YouTube baada ya rapa Rosa Ree kulalamika ulitumia mdundo wa wimbo wake wa Kanyor Aleng bila idhini yake hivyo alikiuka taratibu za hakimiliki.


Huo ulikuwa ni wimbo wa pili kwa Harmonize kuondolewa YouTube kutokana na mdundo wake kuonekana kunakiliwa kutoka kwenye wimbo mwingine. Wa kwanza ni Uno ambao prodyuza wa Kenya, Magix Enga alipeleka malalamiko yake kwenye mtandao huo kisha wakauondosha kwa muda.

Cc; @sifaelpau

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad