6/11/2022

Hatimaye Wachezaji Chama, Bwalya Warejea Mazoezini Simba

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Chama anarejea mazoezini akiwa na kikosi hicho kutokana na kuuguza majeraha tangu alipocheza mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara Desemba 11, mwaka jana dhidi ya Yanga uliomalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya 0-0.
VIUNGO wa Simba, Clatous Chama na Rally Bwalya wameungana na timu hiyo katika mazoezi yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mo Simba Arena ikiwa ni siku moja tangu warejee nchini.

Chama alirejea jana akitokea kwao Zambia kwa ajili ya kumbukumbu ya mwaka mmoja ya kifo cha mkewe, Mercy Mukuka kilichotokea Mei 29, mwaka jana.

Naye Rally Bwalya alitoka kwenye majukumu ya timu yake ya Zambia iliyokuwa inajiandaa na michezo ya kufuzu AFCON mwakani Ivory Coast.

Chama anarejea mazoezini akiwa na kikosi hicho kutokana na kuuguza majeraha tangu alipocheza mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara Desemba 11, mwaka jana dhidi ya Yanga uliomalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya 0-0.


Wachezaji waliofanya mazoezi ni, Aishi Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Ahmed Feruzi, Pascal Wawa, Mohamed Hussein 'Tshabalala', Gadiel Michael, Israel mwenda, Joash Onyango, Kennedy Juma na Henock Inonga.

Wengine ni Clatous Chama, Rally Bwalya, Kibu Denis, Jimmyson Mwanuke, Mzamiru Yassin, Taddeo Lwanga, Pape Sakho, Sadio Kanoute, Erasto Nyoni, Yusuph Mhilu na John Bocco.

Simba iliyopo chini ya Kaimu Kocha wake Mkuu, Seleman Matola baada ya Kocha Mkuu Pablo Franco kutimuliwa Mei 31, mwaka huu inajiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City Alhamisi hii ya Juni 16, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger