6/03/2022

January Makamba Aomba Radhi Kuchelewa Bungeni, Aeleza Sababu

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPAWaziri wa Nishati January Makamba amelazimika kuomba radhi ndani ya Bunge kufuatia kusababisha bunge kusimama kwa dakika 30 asubuhi baada ya yeye na Naibu Waziri wake Stephen Byabato kutokuwepo bungeni wakati mjadala wa wizara hiyo ukiendelea
Waziri Makamba ameeleza kuwa kutokana na uzito wa hoja zilizotolewa na wabunge hao jana iliwalazimi yeye na Naibu wake kuamkia katika kikao cha kutafuta majibu ya hoja zao huku wakiamini kuwa muda wa maswali na majibu utamalizika saa nne na robo asubuhi na badala yake ukamalizika kabla ya saa nne

"Kosa tulilofanya ni utabiri na tulichojifunza ni utabiri, utabiri kwamba maswali huwa yanaisha saa nne na dakika 10 au 15 kutokana na uzoefu wetu, kumbe leo yameisha kabla ya saa nne, kwahiyo tunaingia tunapishana na msafara unatoka, tukatamani kuingia chini ya viti, lakini tunashukuru kwa uelewa wa bunge na tumejifunza kuanzia leo hatutatabiri tena" ameeleza Makamba
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger