6/05/2022

Job Ndugai Afunguka Kuhusu Hali yake "Mimi ni Mzima"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPAKondoa. Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai amesema yeye ni mzima na wala watu wasiwe na wasiwasi wowote.

Ndugai amesema hayo leo June 5, 2022 Wilayani Kondoa wakati wa ibada ya uwekaji wa wakfu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Paulo Mtume kwa wamataifa.

Ibada hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu (Kazi Maalum), George Mkuchika, Mbunge wa Kilosa, Profesa Paramagamba Kabudi, Katibu Tawala wa Dodoma, Dk Fatma Mganga na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dk Hamis Mkanachi.
Mbunge huyo wa Kongwa alipewa nafasi ya kuzungumza na Askofu wa Dayosisi ya Kondoa Dk Giben Gaula.

Akiwa na mkewe Dk Fatma Mganga Ndugai amesema:

"Mimi sijambo kabisa wala msiwe na wasiwasi wowote nimwachie Mama azungumze (Fatma Mganga) kwani yeye ndio kiongozi,".
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger