6/20/2022

Jose Chameleone azungumza baada ya kukamatwa nchini Afrika Kusini

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Haikuwa wikendi njema au tamasha ya kufana kwa mwanamuziki wa Uganda Jose Chameleone baada ya kukamatwa nchini Affrika Kusini.

Hii ni baada ya mmoja wa waandalizi wa tamasha nchini humo kumshtaki kwa polisi.

Bi. Zaina Muwonge ambaye anaendesha kampuni kwa jina Sezana promotions anasemekana kuandaa tamasha nchini Afrika Kusini mwaka 2015 ambapo Jose Chameleone alistahili kutumbuiza lakini akakosa kufika hata baada ya kupokea malipo.

KUlingana na duru za habari,Maafisa wa polisi wanasemekana kutoa msanii huyo kwenye hoteli katika eneo la Sandton muda mfupi kabla ya wakati wa kupanda jukwaani Jumamosi usiku.


 
Chameleone aliashiria kuwepo kwa mzozo pale ambapo aliandika kwenye mitandao ya kijamii maneno haya bila maelezo zaidi;

“Yote haya yanafanywa ili kunitishia na kukwaza mganda mwenzako kwa ajili ya ubinafsi? Haifai kuwa hivyo. Mashabiki zangu wa Afrika Kusini tusalie kuwa imara na tuache muziki uzungumze. Kwa nini tusimamishe onyesho la leo?”

Mwaka 2018 mwezi Januari, Zaina Muwonge aliweka kesi mahakamani kuhusu swala hilo ambapo kupitia kwa mawakili wake Lukwago & Company alikuwa anataka afidiwe na Chameleone pesa ambazo alimlipa kisha akakosa kufika kwenye tamasha.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger