6/13/2022

Joyce Kiria "Ukizingua Nakuzengua Mimi Sing'ang'anii Mahusiano Ambayo Hayana Amani, Silei Upumbavu"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


By Joyce Kiria - "Ivi kwanini Mwanaume akitaka kumwacha mwanamke ni chap kama upepo… hajiulizi ulizi maswali wala hageuki nyuma… ila mwanamke kumwacha mwanaume ni kipengele, hata mahusiano yake yampe stress kiasi gani bado atajaribu kung’ang’ana, atahaha atasumbua watu na mavikao, ataenda kwa waganga, atamaliza makanisa yaani mradi anataka kushikilia ndoa ambayo haina tena furaha na amani why??? 🤷🏽‍♀️🤷🏽‍♀️


mimi niko tofauti sana, ndoa ya kwanza nilipoona sielewielewi kwa kifupi sikuwa najua maana ya ndoa sikujipanga niliondoka 🙌🏽 inahitaji ujasiri


Ya pili, nilipogundua mwenzangu anani-cheat nilimkalisha chini nikamwambia sioni haja ya kuendelea na ndoa yetu kwa sababu yeye kashaanza mahusiano na mtu mwingine, na mimi sio mwanamke ambae nitaweza kuhimili mwanaume wangu kuwa na mwanamke nje, nikamwambia nampa ruhusa aendelee nae, mimi aniwache nipambane tuu na hali yangu, alifikiri namtania,


nikamwambia asinifatilie tena, aniache yeye aendelee na huyo mwanamke wake na akitaka amuoe ili waishi kwa uhuru, lakini nikamwambia sitaki anifatilie, yaani ingawa tunaishi wote kila mtu amaindi maisha yake huku tukifanya mpango wa kutengana tubaki kama wazazi kulea watoto…


Sasa haya mambo ya mabavu ya wanaume wetu, wamezoea ku-cheat na wanawake wengine alafu wake zao hawafanyi kitu, so nadhani alifikiri na mimi ni dizaini hizo, weeee, akaanza kutaka kuni-control kama mkewe wakati nishajua yeye anani-cheat 🙄 nilimwambia oya temana na mimi chaliangu, kila mtu afanye maisha yake, acha kunifatafata,


siku moja nikatoka zangu kunywa wine na rafiki zangu, si akaja kibabe eti mke wa mtu hauko nyumbani mpaka saa sita usiku, kumbuka yeye kulala nje ilikuwa kawaida ila mimi kukaa mpaka saa sita ikamuuma, na nilishamwambia mahusiano yaishe kila mtu afanye yake tulee tuu watoto, akanizaba bao🙄 ndo moto ule ukawaka nikamchamba na huo ndo ukawa mwisho wetu 🙌🏽🙌🏽


MIMI SING’ANG’ANII MAHUSIANO AMBAYO HAYANA AMANI WALA FURAHA, SILEI UPUMBAVU WA AINA YOYOTE.. UKIZINGUA NAKUZINGUA


Ps: sasa huyo ni mimi pls usiniige niachie maisha yangu, mie sitakagi ujinga ujinga, hawa mtawalea nyie sio mimi 🙌🏽 ukija kwenye maisha yangu lazma tuheshimiane 🙌🏽 Ndoa sio lazima

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger