6/15/2022

Kimeumana... Mkuu wa Mkoa Feki Mikononi Mwa Polisi

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Mtu mmoja Warren Max Mwinuka (20), anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya kwa tuhuma za kujifanya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Zuberi Homera.


Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, SACP Ulrich Matei amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa baada ya kutumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram wenye jina linalosomeka juma_homera.


“Mtuhumiwa Warren alikamatwa Juni 7, 2022 maeneo ya Mama John Jijini Mbeya, na alikuwa akitumia akaunti hiyo kuwahadaa watu kwa kujifanya ni Mkuu wa Mkoa na kutoa namba yake ya simu ili kupokea, kutoa, kupeleka kero na shida mbalimbali,” ilisema taarifa hiyo.


Mtuhumiwa Warren Mwinuka mkazi wa eneo la Makondeko jijii Mbeya anatarajia kufikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger