6/18/2022

Kocha Matola Ataka Mchezaji Kibu Dennis avumiliwe

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


KOCHA Msaidizi wa Simba, Selemani Matola amewataka mashabiki wa klabu hiyo kumvumilia mchezaji wao, Kibu Dennis kutokana na kuonekana kushindwa mara kwa mara kumalizia kufunga mabao.

Akizungumza mara baada ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya timu hiyo dhidi ya Mbeya City, ikiondoka na ushindi wa mabao 3-0 juzi usiku kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Matola alisema ni kweli Kibu amekuwa akikosa baadhi ya nafasi za wazi za kufunga mabao, lakini anaamini kuwa anafundishika na baadaye atakuja kuwa mfungaji mzuri.

"Unajua siku zote sisi walimu tunaumia kama timu haitengenezi nafasi, lakini kama unatengeneza na mchezaji anakosa hilo linakuwa ni suala binafsi, unajua Kibu huwa tunakaa naye na kumweleza, pia tunamfanyisha mazoezi ya kufunga, nafikiri taratibu taratibu atabadilika, atafunga na kuwa mfungaji mzuri." Alisema Matola.

Kwenye mechi ya juzi, alikosa mabao mawili ya wazi ambayo kama angekuwa makini au kutulia, Simba ingeweza kutoka na ushindi mnene kwa mabao 5-0.

Mashabiki wa soka nchini, wa Simba na Taifa Stars wamekuwa wakimlaumu mchezaji huyo kutokana na kukosa nafasi za wazi.


Hata hivyo, mchezaji huyo amekuwa akipendwa sana wa makocha mbalimbali kutokana na uwezo wao mkubwa wa kukaa na mpira bila kunyang'anywa kirahisi, kujituma, kusaidia kukaba, na pamoja na kuwa msumbufu mno kwa mabeki, hivyo kuwarahisishia wenzake kazi, hali inayosababisha wawe wanapata nafasi kwenye vikosi vyote viwili, Simba na Taifa Stars.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger