6/06/2022

Kumekucha..Timu ya Biashara United yamtimua Kocha

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


ZIKIWA zimebaki mechi nne ambazo zitaamua timu ya Biashara United kubaki Ligi Kuu Bara au kushuka daraja uongozi wa timu hiyo umefanya maamuzi magumu.

Unataka kufahamu imeamua nini iko hivi; wamemtimua kocha wao mkuu Vivie Bahati ambaye alichukua mikoba ya Patrick Odhiambo ambaye alitimkia Tanzania Prisons.

Katibu Mkuu wa Biashara, Haji Mtete amethibitisha kuondolewa kwa kocha huyo kwenye benchi lao la ufundi akikiri kuwa ni mwendelezo wa matokeo mabaya.

“Ni kweli tumeamua kuachana na kocha Vivie kutokana na mwendelezo wa matokeo mabaya ndani ya timu tumeamua kufanya hivyo baada ya makubaliano ya pande zote mbili,” alisema na kuongeza;

“Haijawa rahisi kwatu kuchukua uamuzi huo kutokana na kubakiza michezo michache ambayo itaamua hatma yetu msimu ujao,” alisema.

Biashara United ipo nafasi ya 15 kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 26 na kufanikiwa kukusanya pointi 24.
HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger