6/01/2022

Kutana na Mwanamke Aliyekufa Akitazama TV na Kugunduliwa Baada ya Miaka Mitatu TV Ikiwa Bado Inawaka

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

Kutana na hiki kisa cha Mwanadada Joyce Carol Vincent raia wa Uingereza ambaye mwili wake ulikutwa sebuleni kwake tayari ukiwa mifupa mitupu kwenye Kochi baada ya kufariki dunia miaka miwili nyuma pasina mtu yeyote kufahamu. Joyce alifariki Disemba 2003 lakini hadi leo sababu ya Kifo chake imebaki kuwa kizungumkuti.

Mwili wake ulikutwa ndani January 25 mwaka 2006 huku Televisheni ambayo alikuwa akitazama, ikiwa bado inawaka pamoja na taa za sebuleni. Kwenye Friji lake kulikutwa bidhaa za mwaka 2003 zikiwa tayari zimekwisha muda. Uchunguzi unaeleza kwamba kabla ya Kifo chake, Joyce alifuta mawasiliano ya kila mtu ambaye anafahamiana naye.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger