6/22/2022

Kwa Konde Boy, Kajala Masanja Hawezi Kuwa BOYA...Chezea Renji Black And Wait

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Dunia iliyoamua Mondi azae na Zari, Hamisa na Tanasha. Ndiyo iliyoamua Queen Kajala, arudi kwa Konde Boy. Dunia ya sasa inaendeshwa na pesa. Uchawi peleka kwenu.


'Renji Blaki & Waiti'. 'Pleti namba' na kadi zote ni umiliki wa jina la Kajala. Konde anataka mtoto awe mmliki halali. Huyo Kajala mnamchukuliaje kwa mfano?


Akatae ili? Wapi huko ambako kuna 'boi frendi' malaika siku hizi? Unataka Msukuma akatae hivi una akili kweli? Sio ajabu 'ulikomenti' alikatae huku ukitumia bando la 'eksi' wako.


Na wigi la elfu 5 alilokununulia ili tu mrudiane. Leo unataka Kajala akatae 'Renji Rova'? Kuweni na akili basi. Hii dunia siyo ile dunia yenu ya utu una thamani kuliko pesa.


Dunia hii pesa ndo ina thamani kuliko utu. Utu 'mai futi'. Acha mtoto mzuri amwagilie moyo. Utadhani 'Renji' ni sawa na bando la jero kwamba kila mtu analo? Konde anaitafuta furaha ilipo.


Kumbuka furaha hutafutwa, matatizo yanakuja yenyewe. Furaha yake ndo ile, kuishi kando ya kiumbe pendwa. Na kiumbe aina ya Kajala anastahili kupiganiwa namna ile.


Ukivuka miaka 30, una muda mfupi wa kuishi kuliko muda ulioishi. Leo hii Kajala ana 40, aendelee kusubiri matatizo badala ya kuitafuta furaha? Maisha ni haya haya. Tuishi!


Imeandikwa na ✍️ @officialtinana

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

1 comment:

  1. sawa kabisa Kajala raha jipe mwenyewe maisha yenyewe mafupi halafu ukatae kula raha kisa??? upe moyo wako kitu inapenda!!!

    ReplyDelete

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger