6/08/2022

Lulu Diva Amwaga KILIO Redioni "Kwanini Juhudi Zangu Zinaonekana Kama Ujinga? "

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Mwimbaji @luludivatz amejikuta akiangua kilio LIVE kwenye redio wakati akifanya mahojiano na Leo Tena ya Clouds FM leo, hii imekuja kufuatia kilichosemwa Jana bungeni na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Hamis Tale Tale (@babutale) ambaye alimtolea mfano Lulu Diva mbele ya Kassim Mganga kwenye hoja yake kuhusu COSOTA na uchache wa Mirabaha kwa wasanii. Babu Tale aliikosoa COSOTA kwa kushindwa kulinganisha vigezo vya wasanii katika mgawanyo wa mirabaha.

Kama Mtoto wa kike mifano kama hiyo hainijengi, Kwanini Juhudi zangu zinaonekana kama ujinga , juhudi hizi ndio zimenifanya nimtibu mama yangu mpaka akafariki, nani ambae hajaoni juhudi zangu katika mziki?

“Mimi nina msanii wangu anaitwa Kassim Mganga, hakuna asiyeimba nyimbo zake kwenye msimu wa harusi. Kassim Mganga unamuita unampa Mrabaha TSh. 50,000. Halafu unamuita Lulu Diva unampa TSh. 550,000, umetumia vigezo gani?” Hamis Tale Tale, Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger