6/17/2022

Simba SC yatangaza rasmi kumuuza kiungo wake Left Footer Magician Rally Bwalya

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Klabu ya Simba yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi Jijini Dar es salaam leo Juni 17 2022, imetangaza rasmi kumuuza kiungo wake Left Footer Magician, Rally Bwalya raia wa Zambia.


"Tumefikia makubaliano ya kumuuza mchezaji wetu Rally Bwalya". Imeeleza kwa ufupi taarifa hiyo kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter.


Kufuatia taarifa hiyo, mchezo wa Jumapili Simba SC dhidi ya KMC utatumika kumuuaga Kiungo huyo Left Footer Magician Rally Bwalya, mtaalamu wa pasi za kudondosha nyuma ya mabeki.


klabu ya Simba haijaweka wazi Ada na klabu yake mpya ambayo anakwenda kuitumikia, ilielezwa ni kutokana na matakwa ya kimkataba, hata hivyo Bwalya amekuwa akiwindwa na Amazulu FC ya Afrika Kusini.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger