Matola aomba sapoti ya viongozi na mashabiki kuiongoza Simba

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Matola aomba sapoti ya viongozi na mashabiki kuiongoza Simba
BAADA ya uongozi wa Simba kumfuta kazi aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Pablo Franco, Kocha msaidizi Seleman Matola amesema yupo tayari kuiongoza timu hiyo mpaka mwisho wa msimu.

Akizungumza na Spotileo, kocha huyo amesema ujuzi aliochota kutoka kwa makocha wengi aliofanya nao kazi akiwa timu hiyo pamoja na uzoefu wake kwenye ligi ya Tanzania Bara, vinampa kiburi cha kuamini anaweza kufanya kazi hiyo.

"Naushukuru uongozi wa Simba, kwa kunipa nafasi hii ya kuiongoza timu katika nafasi ya kocha mkuu kwa mechi tano zilizobaki kabla msimu kumalizika.Nipo tayari kubeba jukumu hili kutokana na uzoefu niliokuwa nao, cha msingi ni sapoti kutoka kwao na mashabiki pia," amesema Matola.

Matola amesema hawezi kuzungumzia maamuzi yaliyofanywa na uongozi wa timu ya kumfuta kazi bosi wake Pablo Franco sababu hilo halimhusu.


 
Amesema kitu cha msingi kwa sasa ni kuanza mikakati ya kuijenga timu ili msimu ujao irudi kwenye ushindani na kurudisha mataji yote ambayo imeyapoteza msimu huu.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad