Mayele, Fei Toto watengewa mamilioni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



 
NYOTA wa Yanga akiwamo kinara wa mabao wa Ligi Kuu Bara, Fiston Mayele na kiungo aliyeitemesha Simba ubingwa wa ASFC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ wametengewa zaidi ya Sh200 milioni kama motisha ya kulibeba kombe hilo la Shirikisho.

Mbali na kuwatengea nyota wake mamilioni hayo, mabosi wa Yanga pia wamepanga kuhamishia sherehe za ubingwa wa Ligi Kuu Bara na pamoja na ASFC (kama wataubeba mbele ya Coastal Union) kutoka jijini Dar es Salaam hadi Arusha wakitaka wakabidhiwe yote huko.

Tuanze na ishu ya mamilioni. Yanga inalipigia hesabu taji la ASFC iliyotwaa mara ya mwisho msimu wa 20150-2016 kwa kuhakikisha inashinda mechi ya fainali dhidi ya Coastal itakayopigwa Julai 2 na kuamua kutenga zaidi ya Sh200 milioni ili kuwapa mzuka mastaa wake.

Habari kutoka ndani ya Yanga zinasema kuwa bilionea wa klabu hiyo, GSM amewatengea kina Mayele kitita cha Sh200 milioni, huku wadau wengine nao wakianza kupekua mifukoni ili kuongeza noti zaidi ili kuhakikisha Julai 2, Yanga inabeba taji hilo litakalounganishwa na la ligi.


 
“GSM keshaweka wazi kwamba atatoa Sh200 milioni kwa mastaa wa timu hiyo kama watabeba ubingwa huo uliokuwa unashikiliwa kwa misimu miwili mfululizo na Simba, lakini kuna vigogo wengine nao wamesema wataongezea mzigo ili Yanga imalize na heshima msimu huu,” kilisema chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya klabu hiyo.

Kwa upande wa sherehe za ubingwa ni kwamba uongozi wa Yanga umeiomba Bodi ya Ligi (TPLB) kuwakabidhi taji la Ligi Kuu litakalounganishwa na lile la ASFC kama watashinda mechi yao ya fainali dhidi ya Coastal katika mechi itakayopigwa jijini Arusha.

Kabla ya fainali hiyo, Yanga itamaliza mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar iliyopangwa kupigwa Juni 29 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, lakini mabosi hao wameomba mchezo huo upelekwe Arusha na bodi imewakubalia.

Mmoja wa viongozi wa Yanga, aliliambia Mwanaspoti walituma ombi hilo kwa vile muda wa mechi ya mwisho ya ligi na fainali ya ASFC zitapishana kwa muda mchache, hivyo wanaona ni vyema wakacheza na Mtibwa Arusha na kukabidhiwa taji lao huko.

Kama Yanga itabeba taji la Ligi Kuu Bara kupitia mechi nne zilizosalia zikiwamo dhidi ya Coastal Union itakayopigwa Juni 15, kisha Polisi Tanzania, Mbeya City na hiyo ya Mtibwa, kisha ikatwaa ASFC itakuwa ni tai la tatu kwao kuwapora Simba msimu huu.

Awali Yanga iliivua ubingwa wa Ngao ya Jamii, Simba kwa kuifumua bao 1-0 lililowekwa kimiani na Fiston Mayele katika mechi iliyopigwa Septemba 27 mwaka jana, japo watani wao nao ililibeba Kombe la Mapinduzi 2022, baada ya kuifumua Azam klatika mchezo wa fainali ya michuano hiyo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad