Mbappe ataka watu 14 waondoke PSG, Neymar, Pochettino ndaniMshambuliaji wa klabu ya Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe ameripotiwa kuwa na orodha ya watu 14 ambao anataka waondoke ndani ya timu hiyo akiwemo Kocha wake Mauricio Pochettino na Neymar.

Kinda hilo lenye umri wa miaka 23 pekee, Mbappe mapema wiki iliyopita alisaini mkataba mpya na PSG ambao umempa mamlaka makubwa mno ili kuachana na mpango wake wa kujiunga na Real Madrid huku kandarasi hiyo ikimuhakikishia kitita kizito cha paundi 650,000 kwa wiki ndani ya matajiri hao wa Ufaransa.

Mbappe amepewa mamlaka makubwa hata katika sajili zitakazofanyika PSG na hivyo inadaiwa Mfaransa huyo anaanza na dirisha hili.

Kwa mujibu wa Mundo Deportivo, ajira za watu 14 zipo mashakani kutokana na mshindi huyo wa Kombe la Dunia anahitaji kukisafisha kikosi cha PSG.

Panga la Mbappe linawahusu viungo Julian Draxler, Ander Herrera, Idrissa Gueye, Mauro Icardi, Leandro Paredes​ ana Thilo Kehrer.

Wengine ambao wapo kwenye orodha ya Kylian Mbappe ni pamoja na Danilo Pereira, Layvin Kurzawa, Pablo Sarabia​, Juan Bernat, Colin Dagba​ na Sergio Rico

Imeandikwa na @fumo255
______

Usikose Elimu ya pesa ni muhimu mno,na zaidi ukilipia Tsh 1000 ebook hapo Chini unaweza kushinda Tsh Laki moja bofya HAPA 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Below Post Ad