6/13/2022

Mchina wa Miaka 42 Anatafutwa Kwa Mauaji

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta mtuhumiwa Zheng Lingyao (42), raia wa China na mkazi wa jiji hilo kwa tuhuma za kumuua Fu Nannan (26) raia wa China mfanyabiashara na mkazi wa Kalenga Ilala, uchunguzi umebaini kulikuwa na tatizo la masuala ya mapenzi

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 12, 2022, na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, ACP Jumanne Muliro, ambapo amesema tukio hilo imetokea Juni 11, 2022, mtaa wa Kalenga Ilala, kwenye ghorofa ya tatu ya wapangaji majira ya saa 5:40 usiku.

"Mtuhumiwa anayetafutwa alifika eneo hilo na kumjeruhi kwa risasi tumboni Nie Mnqino (32) raia wa China na baadaye alimfyatulia risasi Fu Nannan alipoteza maisha na Nie anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, uchunguzi wa awali wa tukio hili umebaini kuwepo kwa tatizo la kutoelewana lililotokana na masuala ya kimapenzi,"amesema Kamanda Muliro

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger