Mdee aibana Serikali madeni ya mifuko ya hifadhi, Serikali yatoa maelezo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Dodoma. Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Mdee ameibana Serikali akitaka kujua mpaka sasa inadaiwa kiasi gani cha fedha ambazo imekopa kutoka Mifuko ya Hifadhi za Jamii.

Mdee katika swali lake bungeni leo Jumanne Juni 14, 2022 pia amehoji ni kiasi gani cha madeni kimeshalipwa na kwa utaratibu gani.

Akijibu maswali hayo kwa pamoja, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Hamad Hassan Chande amesema Serikali ilikopa fedha kutoka katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Chande amesema deni la michango ya wastaafu waliokuwa katika utumishi kabla ya mwaka 1999 na kutaja mchanganuo wa madeni na kiasi kilicholipwa.


 
Naibu Waziri huyo amesema Mfuko wa PSSSF ni Sh506.88 bilioni na imeshalipwa Sh500 bilioni ambazo zimelipwa kwa utaratibu wa kibajeti.

Kuhusu michango ya wastaafu waliokuwa katika utumishi kabla ya mwaka 1999 amesema zilikopwa Sh4.46 trilioni huku zikiwa zimelipwa Sh2.17 trilioni kwa utaratibu wa hatifungani maalumu.

“Aidha kiasi kilichobaki cha deni la mfuko wa PSSSF Sh6.88 bilioni na michango ya wastaafu Sh2.29 trilioni, zitalipwa katika bajeti ya mwaka 2022/23,” amesema.


Amesema kwenye mfuko wa NSSF Sh292.59 bilioni zilizokidhi vigezo baada ya uhakiki wa deni la Sh490.16 bilioni zitalipwa katika bajeti ya mwaka 2022/23 wakati mfuko wa NHIF Sh80.68 bilioni zilizokidhi vigezo baada ya uhakiki wa deni la Sh209.72 bilioni zitalipwa katika bajeti ya mwaka 2022/23.

Kwa mujibu wa Chande, Serikali itaendelea kuhakiki sehemu iliyobaki ya deni la Mfuko wa NSSF na NHIF ili yaweze kujumuishwa katika mpango wa malipo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad