6/10/2022

Mdogo wa Prof Jay "Kwa Sasa Anaongea na Amefurahi kupewa Tuzo, ile Tuzo ilimpa faraja kubwa sana"

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA

 


Ni wengi walisikitika waliposikia hali ya afya ya Legend wa Bongofleva Joseph Haule Profesa Jay aliyelazwa Hospitalini kwa siku 127 haikuwa nzuri kiasi kwamba hata kuongea hakuwa anaweza, sasa baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali Familia yake imethibitisha kwamba Prof Jizze anaongea.


"Sasa hivi anaongea ila kwakuwa amekaa Hospitali sana hana nguvu kabisa anakuwa kachoka kwahiyo hata kumuongelesha hatupendi sana ili tusimchoshe"


"Amefurahi kupewa Tuzo, ile Tuzo ilimpa faraja kubwa sana nilipompelekea pale kitandani aliipokea akaikumbatia akaibusu hata Mimi nilimuona amefurahi sana pengine iliweza kumuongezea hata nguvu" ——— amesema Msemaji wa familia Black Rhino @blackchatta ambaye ni Mdogo wa Profesa J.


Hospitali ya Taifa Muhimbili leo imethibitisha Profesa J kuruhusiwa kutoka Hospitalini jana baada ya afya yake kuimarika ambapo Familia yake imesema kwa sasa yuko sehemu akipatiwa uangalizi maalum na sio nyumbani kwake.

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger