6/10/2022

Meneja wa Harmonize Chopa Atoa Ufafanuzi Tetesi za Meneja Mjerumani Kuondolewa Konde Gang Kisa Kajala

JIUNGE NA GROUP LA TELEGRAM LA AJIRA YAKO KUPATA AJIRA MPYA ZINAZOTANGAZWA KILA SIKU BONYEZA HAPA


Meneja wa msanii Harmonize  , Chopa ametolea ufafanuzi juu ya kile kilicho tokea kwenye Bio ya meneja mwenzie kwa Harmonize na Konde Gang kiujumla, Mjerumani (siku ya Jana june 8) ambaye alifuta kila kitu kuhusiana na masuala ya Konde Gang kwenye Bio yake ya Instagram kabla hajaiupdate tena, kitu ambacho kimeleta sintofahamu kwa wengi huku wakihisi Mjerumani kajitoa KGMW, na ujio wa Kajala Masanja Kama C.E.O pale Konde Gang ndio sababu.

Hasa Kupitia Empire ya EFM, Chopa amedai kilicho tokea ni kuwa Mjerumani alikuwa anaedit baadhi ya vitu kwenye Bio yake lakini kabla hajasave akawa offline, na matokeo yake ni kile kilichoenda mitandaoni, Chopa amekazia kuwa Mjerumani bado ni Meneja wa Harmonize na Konde Gang na pia amefurahi kuona, mwanamke mwenzie (Kajala) kuwa kwenye uongozi wa Label hiyo.

Hivi ukiedit Bio na ukatoka online bila kusave, si inabaki kama ilivyo kuwa awali ama?

HABARI HIZI ZINAPATIKANA KWENYE APP YA UDAKU SPECIAL, BONYEZA HAPA KUIDOWNLOAD KWENYE SIMU YAKO
Share:

0 Blogger:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL | Powered by Blogger