Mgombea Urais azomewa nyumbani kwake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA




KIONGOZI wa chama cha Wiper nchini Kenya, Kalonzo Musyoka, amekutana na udhalilishaji akiwa jukwaani baada ya kundi kubwa la wananchi wanaomsikiliza kumzomea akifanya kampeni katika kaunti yake ya nyumbani ya Kitui jana tarehe 17 Juni, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kalonzo alilazimika kuvumulia hali hiyo katika soko la Ikutha nchini humo alipozomewa mara kadhaa na kulazimika kukatiza hotuba yake.

Umati huo uliotamka ‘kwenda huko’ ulikuwa ukipinga juhudi zake za kumfanyia kampeni mbunge wa Kitui Kusini na mgombea wa chama cha Jubilee, Racheal Kaki Nyamai na kusisitiza kuwa mgombea wa ODM, Onesmus Mumo King ndiye awe mzumngumzaji badala yake.

Wakati hayo yakiendelea, Mgombea mwenza wa William Ruto kupitia tiketi ya UDA Rigathi Gachagua naye alipagwa butwaa alipokuwa akifanyia kampeni ya Muungano wa Kenya Kwanza katika eneo la Githunguri, Kaunti ya Kiambu.

Gachagua alipata wakati mgumu kutuliza umati baada ya kuwashambulia Rais Uhuru Kenyatta na Azimio La Umoja One na mgombea urais wa chama cha Muungano wa Kenya, Raila Odinga.

Baadhi ya umati ambao haukutaka kusikia lolote walielezea kukerwa kwao na mashambulizi yake dhidi ya wawili hao na kumshutumu kwa kutomuheshimu rais na Raila.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad